RAIS MAGUFULI ATEUA WANNE, NI WAKURUGENZI NA WENYEVITI.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi ameeleza kuwa Rais Magufuli amemteua Prof. Lazaro S.P. Busagala kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomiki ( TAEC ) kuanzia tarehe 22 March, 2018. Prof Lazaro S.P. Busagala alikuwa Makamu Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara ( CBE ) kitivo cha Taaluma na Utafiti. Prof. Damian Gabagambi ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo la Taifa ( NDC ) kuanzia tarehe 22 March, 2018 . Prof. Gabagambi anachukua nafasi ya Mlingi Elisha Mkucha ambaye atapangiwa kazi nyingine. Kabla ya uteuzi Prof. Gabagambi alikuwa Mhadhiri wa Uchumi wa Chuo Kikuu cha Kilimo, Sokoine ( SUA ). Rais Magufuli amemteua Dkt. Deodatus Michael Mutasiwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali ya Benjamin Mkapa, Dodoma. Dkt. Alphone Bilola ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa, Dodoma. Kabla ya Uteuzi huu Dkt. Chandika alikuwa...